Waziri wa Mazingira wa Zimbabwe
Oppah Muchinguri amesema daktari wa meno wa Marekani aliyemua Simba
maarufu nchini Zimbabwe anapaswa kurejeshwa kutoka Marekani ili
akabiliane na makosa yake.
Waziri huyo amesema Daktari Walter
Palmer anapaswa kurejeshwa Zimbabwe ili awajibishwe kwa kitendo chake
hicho cha kuvunja sheria.
Daktari Palmer, kutoka Minnesota,
inaaminika kuwa alilipa dola 50,000 ili kuwinda Simba, anayejulikana
kama Cecil, na alidhani kuwa anaruhusiwa kisheria kumua Simba huyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni