Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imetangaza kuwa zoezi la kuchukuwa fomu za wagombe wa urais, ubunge
na udiwani walioteuliwa kuwania nafasi hizo mbalimbali na vyama vyao
vya siasa litaaanza kesho na kukamilika tarehe 21, mwaka huu.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu
Damian Lubuva amewatadhadharisha wagombea watakaokuja kuchukua fomu
kwa shmara shamra kuhakikisha wafuasi wao wanakaa umbali wa mita 400
kutoka katika ofisi hizo ili kuepusha vurugu.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam Kamanda Suleiman Kova, amesema jeshi la
polisi halitamvumilia mgombea yeyote atakayekiuka agizo hilo na
wafuasi wake kusababisha vurugu ama kusababisha baadhi ya shughuli
kutofanyika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni