Mmoja wa wakufunzi wa masomo ya
ujasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Dar es salaam Profesa Humphrey Mushi
akizungumza katika semina ya ujasiriamali inayotolewa na Taasisi ya
utafiti ya vyuo vikuu vya afrika na kusini mwa Afrika ( ESAURP) kwa
wafanyabiashara ndogondogo mkoa wa mbeya katika ukumbi wa shule ya
St. Agrey jijini Mbeya Agosti 24 mwaka huu.
Mwakilishi wa Taasisi ya Esaurp
kutoka jijini Dar es salaam Ndugu Peter Celestine akizungumza katika
mafunzo hayo ya siku tano yaliyolenga kuwapatia wajasiriamli hao
Ujuzi Mbinu ,maarifa pamoja na stadi za biashara ili kuwezesha ukuaji
wa biashara zao.
Baadhi ya wajasirimali kutoka maeneo
tofauti tofauti Mkoani mbeya wakiendelea kupatiwa mafunzo.
Mmoja wa walimu katika mafunzo hayo
Ndugu Upendo Mwinuka akizungumza na wajasirimali hao hawapo Pichani.
Afisa Mikopo kutoka Benki ya Posta
Tanzania Mbeya (TPB) Ndugu Tresphory Mtwele akizungumza na
wajasirimali hao ili kuwashawishi kujiunga katika vikundi ili waweze
kupatiwa mikopo ya riba nafuu na benki hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni