Baada ya kuchezea kichapo jana cha
mabao 2-1 kutoka kwa Swansea, Manchester United, imetenga kitita cha
paundi milioni 36 kumnasa mshambuliaji kinda wa Monaco, Anthony
Martial.
Uamuzi huo umekuja baada ya Javier
Hernandez kuondoka Manchester United hapo jana kujiunga na klabu ya
Ujerumani ya Bayer Leverkusen kwa kitita cha paundi milioni 12.
Timu ya Monaco bado haijakubalia ofa
hiyo kwa mchezaji wao huyo mwenye kiwango cha juu ambaye anafananisha
na Thierry Henry mpya, hata hivyo mazungumzo yanatarajiwa kuendelea
hii leo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni