Aliyekuwa mbabe wa vita Bosco
Ntaganda aliyepachikwa jina la "The Terminator",
atafikishwa mahakamani katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)
jumatano akikabiliwa na mashtaka ua uhalifu wa kivita, ubakaji watoto
uliofanywa na kundi lake.
Kiongozi huyo wa waasi ambaye
alikuwa anaogopwa mno katika eneo la kaskazini mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo anakabiliwa na makosa 13 ya uhalifu wa kivita,
makosa 5 ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Katika kesi hiyo mwendesha mashtaka
wa ICC Fatou Bensouda atakuwa wa kwanza kuongea, akifuatiwa na wakili
wa Ntaganda pamoja na wawakilishi wa wahanga 2,149 watatoa ushahidi
wao katika kesi hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni