.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 20 Agosti 2015

BAADA YA KUZIDIWA KETE LOUIS VAN GAAL SASA AMSAKA SADIO MANE

Baada ya kuzidiwa kete na kocha wa Chelsea Jose Mourinho na kumkosa mshambuliaji wa Barcelona Pedro, kocha wa Manchester United Louis van Gaal sasa ameelekeza nguvu zake kumnasa Sadio Mane wa Southampton.

Tayari timu ya Southampton imekiri kupokea maombi ya Manchester United ya kutaka kumtwa Mane aliyefunga mabao 10 katika michezo 32 ya Ligi ya Kuu ya Uingereza msimu uliopita baada ya kununuliwa kwa kitita cha paundi milioni 10 kutoka Red Bull Salzburg.
Kama hiyo haitoshi van Gaal pia amepigwa kumbo na majirani wake Manchester City baada ya kufanikisha kumtwaa beki wa Valencia Nicolas Otamendi kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 32.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni