Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini
amezuia kuachiwa mapema kutoka gerezani mwanariadha Oscar Pistorius
siku ya kesho.
Amesema uamuzi wa bodi ya msamaha wa
kumtoa gerezani mwanariadha huyo baada ya kutumikia kifungo cha miezi
10 kati ya miaka mitano umetolewa mapema na bila ya kuzingatia
sheria.
Kutokana na uamuzi huo wa Waziri
Michael Masutha, sasa itachukua miezi kadhaa kabla ya bodi kujadili
uamuzi wake.
Pistorius alitiwa hatiani kwa mauaji
bila ya kukusudia mwaka jana baada ya kumpiga risasi na kumuua mpenzi
wake Reeva Steenkamp.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni