Idara ya serikali ya Marekani
imesema rais wa Sudani Kusini ameahidi kutia saini makubaliano ya
amani, ambayo awali alisita kuyasaini.
Rais Salva Kiir amemuambia Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, kuwa ameamua kutia saini
makubaliano ya amani baada ya siku kadhaa za mashauriano.
Kukataa kwake kutia saini
makubaliano hayo siku ya jumatatu ya kumaliza machafuko ya miezi 18,
kulielezwa na msuluhishi mkuu wa mgogoro huo kama mchezo wa kiakili.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni