Aliyevalia shati la blue ni Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia akiondoka katika banda la kampuni ya Simba Cement mara baada ya kutembelea banda hilo katika viwanja vya nane nane Themi jijini Arusha ,kushoto ni Mkurugenzi wa Kenya plant helth inspectorate service Bi.Esther Kimani(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)Hayo yamebainishwa na afisa masoko Mkuu wa kampuni ya Simba Cement ambao ni watengenezaji wa Saruji ,Leslie Massawe wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembea banda lao katika maonyesho ya nane nane ,kanda ya kaskazini jijini Arusha
Massawe alisema kuwa utafiti uliofanywa na kampuni yao ya saruji inaonyesha kuwa baadhi ya wajenzi hawafuati mchanganyiko unaokubalika baina ya saruji,mchanga,kokoto hivyo inapelekea kupata matofali yaliyochini ya kiwango
“Bidhaa zetu ni matokeo ya utafiti wa kina na uboreshaji makini unaofanywa na wataalumu wetu kupitia ujuzi wao wenye sifa zinazozingatia viwango vya ubora wa simenti Tanzania”alisema Massawe
Aidha alisema kuwa wanautarabu wa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wateja wao pamoja na wananchi kwa ujumla juu ya matumizi sahihi ya saruji ,katika ujenzi wa sekta mbalimbali sanjari na uzalishaji wa viwandani hali itakayosaidia upatikaniji wa ujenzi wa nyumba imara na miundombinu bora
Alitoa wito kwa wananchi kupata elimu ya matumizi bora ya vifaa vinavyotumika katika ujenzi kabla ya kuanza ujenzi,huku akiwataka mafundi ujenzi na watengenezaji wa matofali kutenga muda wa kushiriki semina mbalimbali zinazotolewa na kampuni za saruji
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni