Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa (UN), limeishinikiza serikali ya Burundi kuanzisha mara moja
mazungumzo na upinzania ili kukomesha ghasia zinazoelekea
kuitumbukiza nchi hiyo kwenye machafuko.
Wajumbe 15 wa baraza hilo wakiungwa
mkono na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon wametuma
ujumbe wa ngazi ya juu wa umoja huo kujaribu kutuliza mgogoro wa
Burundi.
Baraza hilo limetaka kuwepo
mazungumzo baada ya maafisa waandamizi wa UN kuonya katika mkutano wa
ndani wa dharura ulioitishwa na Ufaransa kuwa machafuko yanazidi
kukithiri katika nchi ya Burundi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni