Hali ya tahadhari imewekwa katika
mji wa Ferguson nchini Marekani huku kukiwa na maandamano ya
kuadhimisha kifo cha kijana Mmarekani mweusi Michael Brown.
Mji huo umeelezwa kuwepo katika hali
ya taharuki baada ya kijana mwingine mweusi kuumizwa vibaya kwa
risasi katika mapambano na polisi siku ya jumapili.
Kijana huyo Tyrone Harris mwenye
umri wa miaka 18, baadae alifunguliwa mashtaka ya kuwashambulia
maafisa polisi. Gavana wa Missouri Jay Nixon ametoa wito wa kutaka
maandamano kuwa ya amani.
Mwanaharakati maarufu Cornel West ni miongoni mwa watu wapatao 20 waliokamatwa



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni