Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria
ameteua kamati ya kumshauri juu ya njia gani nzuri anaweza kuitumia
kukabiliana na rushwa na kufanya mabadiliko ya mfumo wa sheria.
Kamati hiyo ya wajumbe saba wa
kumshauri rais kuhusu kukabiliana na rushwa inaundwa na wanazuoni.
Rais Buhari alichaguliwa mwezi Mei,
aliahidi zaidi kukabiliana na rushwa nchini Nigeria, ambapo amesema
anaamini maafisa wa serikali wameiba karibu dola bilioni 150.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni