Zaidi ya barua pepe 300 kutoka
katika seva binafsi ya Bi. Hillary Clinton zitapitiwa kubaini iwapo
zilikuwa na taarifa za siri za serikali.
Idara ya serikali ya Marekani
ilibaini barua pepe hizo na inaangalia iwapo zinaweza kutolewa kwa
umma.
Bi. Clinton alitumia mail ya binafsi
akiwa waziri wa mambo ya nje katika miaka minne na kuibua wimbi la
kumkosoa kwa kwenda kinyume na taratibu za serikali.
Hata hivyo Bi. Clinton anayewania
urais kwa tiketi ya chama cha Democratic mwakani amesema email yake
haikuwa na nyaraka za siri za serikali kwa wakati huo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni