Waziri Mkuu wa Thailand, Prayuth
Chan-ocha amesema mlipuko wa bomo katika mahala patakatifu katika
Jiji la Bangkok, hapo jana ni tukio baya la mashambulizi kuwahi
kutokea nchini humo.
Shambulio hilo lililofanywa katika
mahala patakatifu pa dhehebu la Erawan Hindu
limeuwa watu 21, wakiwemo raia wa
kigeni huku idadi kubwa ya watu wakijeruhiwa.
Bw. Prayuth amesema wahusika wa
tukio hilo hawajajulikana hata hivyo polisi wanamchunguza mtuhumiwa
mmoja, aliyeonekana kwenye kamera za usalama.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni