Timu ya Barcelona jana usiku
ilishindwa kulipa kisasi cha kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Athletic Bilbao wakiwa katika dimba
la nyumbani la Nou Camp na kujikuta wakikosa ubingwa wa Kombe la
Super baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Nyota wao Lionel Messi alikuwa wa
kwanza kuiandikia Barcelona lakini Athletic walipambana kiume ugenini
na kufanikiwa kulichomoa goli hilo kupitia kwa Aritz Aduriz , huku
Gerard Pique akitolewa nje, na kuifanya Athletic Bilbao kutwaa kombe
hilo kwa mara ya kwanza tangu miaka 31 iliyopita.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni