Waokoaji wanaotafuta manusura wa
ajali ya boti iliyozama bahari ya Mediterranean ikiwa na wahamiaji
600 kutoka Afrika katika Pwani ya Libya wameondoa matumaini ya kupata
watu walio hai.
Maafisa hao awali walihofia kuwa
mamia ya wahamiaji hao watakuwa wamekufa maji, hata hivyo Shirika la
Kuwahudumia Wakimbizi Duniani, UNHCR limesema watu 400 wameokolewa.
Walinzi wa Pwani ya Italia wameeleza
kuwa miili 25 imepatikana hadi sasa hata hivyo haijulikani ni idadi
gani ya watu ambao bado hawajapatikana.
Zaidi ya wahamiaji 2,000 inasemekana
wamekufa katika mwaka 2015 wakijaribu kukatiza baharia ya
Mediterranean kwenda Ulaya.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni