Watu wapatao sita wakiwemo maafisa
polisi watatu wameuwawa katika bomu la kujitoa mhanga mashariki mwa
Afghanistan.
Lori lililojaa milipuko ililipuliwa
nje ya uzio wa polisi huko Puli Alam katika mji wa Logar.
Wapiganaji wa Taliban wamesema
wametekeleza shambulio hilo. Hili ni shambulio kubwa la kwanza tangu
wapiganaji wa kundi hilo kuthibitisha kiongozi wa Mullah Omar
amekufa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni