Baraza la Congress la Peru
limeidhinisha muswada wa sheria ambayo inaruhusu vikosi vya anga vya
taifa hilo kuitungua ndege yoyote watakayoihisi imebeba dawa za
kulevya.
Peru huzalisha cocaine nyingi zaidi
ya mataifa mengine duniani ambapo sehemu kubwa ya dawa hiyo ya
kulevya huingizwa kwa magendo nchini Marekani.
Muswada huo umepitishwa bila
kupingwa unangojea kutiwa saini na rais Ollanta Humala, ingawa
unakabiliwa na upinzani kutoka Marekani kwa kukiuka usalama wa anga.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni