Robin van Persie amefunga bao
akitokea benchi na kuipatia ushindi Fenerbahce kwa bao la dakika za
mwisho pindi tu alipopata mpira kwa mara ya kwanza katika mchezo wa
Ligi ya Uropa dhidi ya Atromitos Anthes.
Goli hilo ni la kwanza kwa Mdachi
huyo kwa klabu yake hiyo ya Uturiki, tangu asajiliwe na klabu ya
Fenerbahce akitokea Manchester United.
Akiwa ameingia uwanjani katika
dakika ya 80, huku akiendelea kuhangaika na jeraha la misuli ya
kigimbi cha mguu, van Persie alipachika bao la kichwa katika mchezo
huo uliochezwa nchini Ugiriki.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni