Na Mwandishi Wetu
Bondia bingwa wa Afrika wa mikanda miwili WPBF na UBO Afrika Ibrahimu Class 'King Class Mawe'anapanda tena ulingoni kwa mara nyingine kukabiliana na Ally Muro katika mpambano wake wa kumaliza ubishi nani zaidi kati ya mabondia hao utakaofanyika katika viwanja vya basketball vilivyopo katika shule ya msingi Uhuru Wasichana Kariakoo Dar es salaam. Bondia huyo mwenye historia ya kucheza mchezo mzuri wa masumbwi mithili ya mfalme wa ngumi duniani Mohamed Ali, amekuwa kivutio kikubwa nchini ambapo mashabiki wengi wamekuwa wakimulizia kuwa anacheza lini, hata hivyo jibu limepatikana kuwa anacheza August 22 katika viwanja vya shule ya Uhuru wasichana.
Katika mpambano huo, watasindikizwa na bondia Machachali anayechipukia kwa sasa, Vicent Mbilinyi atakayemenyana na Kelvin Majiba wakati Raymond Mbwago atacheza na Roger Masawe. Husein Pendeza atamalizana ubishi na Shomari Mirundi mipambano yote hiyo ni ya raundi sita.
Lengo kubwa la mchezo huo ni kumpongeza Lulu Kayage bondia pekee wa kike katika ngumi za kulipwa aliyethubutu kuonesha uwezo wake akiwa ugenini na kumpiga kwa T.K.O ya raundi ya pili bondia wa Afrika ya kusini Lizbeth Sivhaga na ndie atakaekuwa mgeni wa heshima katika mapambano hayo
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
Pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni