Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri
amesema jengo la usalama wa taifa kaskazini mwa Cairo limekumbwa na
tukio la mlipuko wa bomu kwenye gari mapema leo.
Maafisa polisi sita wamejeruhiwa na
mlipuko huo kaskazini mwa Wilaya ya Shubra katika Jiji hilo, hakuna
taarifa za kutokea vifo.
Wakazi katika Jiji la Cairo
wameripotiwa wakisema wamesikia mlipuko mkubwa. Kumekuwepo na matukio
kadhaa ya mashambulio ya wapiganaji wa Kiislam katika mwaka huu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni