Polisi nchini Kenya wamewataja
wanaume watatu ambao wanadai kuwa wamekuwa wakihusika na
kuwaandikisha vijana kujiunga na vikundi vya ugaidi.
Watu hao Abdifatah Abubakar Ahmed,
Ramadhan Hamisi Kufungwa na Ahmed Imam Ali ingawa awali walikuwa
wakifanya shughuli zao Kenya, hivi sasa wamekimbilia nchini Somalia
ambayo ni kitovu cha ugaidi.
Watuhumiwa hao watiifu wa kundi la
Al Shabaab wametuhumiwa kwa kuwashawishi vijana kwa njia ya intaneti
wakiwemo wa vyuo vikuu, kwa kuwaahidi fedha nyingi pamoja na mambo
mengine mazuri.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni