Timu ya soka ya Manchester United imeanza vyema ligi kuu nchini England baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham.
Katika mchezo huo, Man U iliwachukua dakika 21 tu ya kipindi cha kwanza kupata bao lililofungwa na mlinzi wa Tottenham, Kyle Walker akiwa katika harakati za kuondoa hatari langoni mwake.
Wachezaji wa Manchester United wakipongezana baada ua kupata bao lililotokana na makosa ya beki wa Tottenham, Walker aliyejifunga.
Aliyekuwa mlinda mlango wa Manchester United, De Gea akiweka saini kwa mashabiki wa timu hiyo. Mlinda mlango huyo anatimkia Real Madrid ya Hispania.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni