Marubani wa ndege ya British Airways
iliyokuwa inaenda Marekani ikiwa na abiria 221 wameugua hafla wakiwa
futi 10,000 angani na kulazimika kutua kwa dharura baada ya njia za
viyoyozi vya chumba chao kuziba.
Marubani watatu walilazimika kutumia
masks za kupitishia hewa ya oxygeni, ili kuweza kutua tena Jijini
London baada ya kusafiri kwa saa moja.
Baada ya uchunguzi ilibainika kuwa
njia za viyoyozi katika chumba cha marubaini zilikuwa zimezibwa na
vipande vya waya, karatasi za kufungia nyaya pamoja na vitu vingine.
Marubani hao watatu walianza kusikia
kuumwa kichwa na kizunguzungu ndipo walipovuta masks za hewa ya
oxygeni na kuomba kutua kwa dharura.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni