.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 17 Agosti 2015

MASHINDANO YA MISS TANZANIA SASA RUKSA




Aidha, LINO imewasilisha muundo wa kamati ya uendeshaji wa shindano yenye muelekeo wa kuzingatia jinsia.

Katika kuboresha na kurudisha hadhi ya shindano la Miss Tanzania, LINO International Agency Limited imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne (4) kwa ajili ya maandalizi ya awali ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakala katika ngazi zote husika.
 
BASATA linapenda kuwafahamisha wadau wote wa Sanaa hususan wale wa shindano la urembo la Miss Tanzania kwamba Kampuni ya LINO imetekeleza maagizo ya msingi iliyopewa kama masharti ya kufunguliwa. 

Na kwamba baada ya kufanyia kazi changamoto zilizokuwa zimejitokeza BASATA limeyafungulia mashindano ya Miss Tanzania kwa masharti ya kukamilisha changamoto zilizobakia.

Ni matarajio ya BASATA kwamba kampuni ya LINO itazingatia taratibu zote za uendeshaji wa matukio ya Sanaa nchini na kwamba haitarudia tena makosa yatakayopelekea kuliweka shindano hili katika hali ya kushuka hadhi na kuzua sintofahamu katika jamii.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza

KATIBU MTENDAJI

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni