Wachezaji wa timu ya Polisi na Simba wakisimama wakati wa kupigwa kwa wimbo wa Usalama wa Raia kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu inayotarajiwa kuaza mwezi ujao.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan. Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan. Kikosi cha timu ya Polisi Zanzibar kilichokubali kipigo cha bao 2--0 kutoka kwa timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Kikosi cha timu ya Simba kilichotowa kipigo cha mabao 2--0 dhidi ya timu ya Polisi Zanzibar wakati wa mchezo wao wa kujipima nguvu wa tatu kisiwani Zanzibar ikiwa imeshinda michezo yake yote.
Kipa wa timu ya Polisi akiokoa mpira golini kwake huku mchezaji wa Simba akiwa nyuma yake
Mchezaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Polisi wakati wa mchezo wao wa kirafiki kujipima nguvu kujiandaa na Ligi Kuu zinazotarajiwa kuaza hivi karibuni Ligi ya Tanzania Bara na ya Zanzibar.
Mchezaji wa Simba akijiandaa kumpita beki wa timu ya Simba, wakati wa mchezo wao wa kirafiki katika mchezo huo timu ya Simba imeshinda 2--0
Wachezaji wa timu ya Simba na Polisi wakiwania mpira
Mshambuliaji wa timu ya Simba akiweka majaro golini kwa timu ya Polisi Picha na OthmanMapara.Blog Zanzinews.com
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni