Mchezaji mpya wa Manchester United,
Memphis Depay aliyenunuliwa kwa paundi milioni 30, ameanza kuonyesha
makali yake baada ya jana kuifungia timu yake mabao mawili dhidi ya
Klabu ya Brugge katika mchezo wa Ligi ya Mabigwa kuwania kuingia
hatua ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Timu ya Brugge ilikuwa ya kwanza
kuiamsha Manchester United baada ya kupata goli la kujifunga Michael
Carrick kufuatia mpira wa adhabu, lakini Depay alisawazisha kwa shuti
la chini la kuzungusha mpira umbali wa yadi 25.
Depay kama haitoshi alifunga bao la
pili kwa shuti la kuzungusha mpira wa juu na kisha kumpigia krosi ya
pande la kichwa Marouane Fellaini aliyetikisa nyavu na kuiandikia
Manchester united bao la tatu.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni