Muda mfupi kabla ya kupulizwa kwa kipyenga cha ligi kuu nchini England, timu ya soka ya Chelsea imempa mkataba mnono wa miaka minne ( 4 ) kocha wake mkuu Mreno, Jose Mourinho wa kuendelea kuifundisha timu hiyo yenye maskani yake jijini London.
Mourinho ambaye msimu uliopita aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi hiyo, amesaini ambao utafikia kikomo mwaka 2019 na atalipwa paundi milioni 30. Msimu uliopita alitwaa vikombe viwili, ligi kuu na Capital One akiwa na timu hiyo.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni