Msaidizi wa karibu wa rais Pierre
Nkurunziza ameuwawa katika shambulio lililofanywa akiwa kwenye gari
lake Jijini Bujumbura.
Msaidizi huyo Jenerali Adolphe
Nshimirimana alikuwa ni mkuu wa zamani wa usalama na mkuu wa vikosi
vya jeshi.
Washambuliaji walililenga gari lake
katika wilaya ya Kamenge wakiwa na bunduki aina ya machine gun pamoja
na kombora la kutungulia roketi.
Burundi imekumbwa na hali ya
machafuko tangu Aprili, bada ya Nkurunziza atangaze kuwani tena urais
kwa muhula wa tatu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni