.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 3 Agosti 2015

KASI YA WAHAMIAJI HARAMU WAIUMIZA KICHWA UINGEREZA

Asilimia 70 ya maelfu ya wahamiaji kutoka bara la Afrika wanaokatiza eneo la Calais Ufanransa kuingia Uingereza wanafanikiwa kufanya hivyo wabunge wa nchi hiyo wametahadharisha.

Takwimu za mkuu wa polisi zimebanisha wahamiaji haramu 900 huingia Uingereza kila mwezi, wakati mawaziri wa nchi hiyo wakiweka jitihada ya kudhibiti hali hiyo.

Mawaziri watatangaza leo hatua za kuwabana wamiliki wa nyumba watakaoshindwa kuhakiki iwapo wanazikodisha nyumba zao kwa wahamiaji haramu ambapo watakabiliwa na hukumu ya miaka mitano jela.
                    Mhamiaji akiwa kajipinda chini ya lori katika kuzamia Uingereza
                            Mhamiaji akiwa amepanda juu ya uzuio katika eneo la Calais

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni