Makumi ya wanaume waliovaa sidiria
na wanawake wameandamana huko Hong Kong baada ya mwanamke mmoja
kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kumtuhumu polisi
mwandamizi mwanaume kumshika titi lake.
Mwanamke huyo Ng Lai-ying, 30, alimtuhumu Inspekta Mkuu wa polisi Chan Ka-po kwa
kumshika titi lake wakati wa maandamano yaliyofanyika mwezi Machi,
mwaka huu.
Hata hivyo mahakama ilimgeuzi kibao
mwanamke huyo, kwa madai kuwa alifanyamakusudi kusogeza titi lake
dhidi ya mwili wa polisi huyo ili baadae amtuhumu kwa kumdhalilisha.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni