Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya MSD ya mwaka 2013/2014 uliofanyika Ofisi za MSD Keko jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imezindua rasmi taarifa yake ya mwaka 2013/2014 (Annual Report), ambayo ilizinduliwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo, Profesa Mtulia alisema kupanda kwa huduma za usambazaji dawa, upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 55 hadi 85 ni jambo la kujivunia.
Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema mpango wa MSD kwa sasa ni kuanzisha maduka ya dawa ambayo yataendeshwa na MSD ambapo kwa kuanzia hivi karibuni litazinduliwa mkoani Mbeya na baadae itafuatia mikoa Kanda za Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni