Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla leo amekagua ujenzi wa mradi mkubwa wa maji kwa ajili ya wakazi wa mji wa Musoma.
Mradi huo unagharimu shilingi bilioni 44 na utazalisha maji lita za ujazo 36,000 wakati mahitaji ya sasa ni lita za ujazo 24,000.
Akiongea mara baada ya kukagua mradi huo kuanzia kwenye chanzo, ulazaji mabomba na matanki, Naibu Waziri wa Maji, Mh Makalla amemwagiza mkandarasi kukamilisha mradi huo mwezi Februari, 2016.
Pia amesema kwakuwa mradi huo una mifumo minne, amemtaka mkandarasi akamilishe mfumo mmoja kwa haraka mwezi wa tisa na maji yasukumwe mjini mwezi Septemba wakati mradi ukisubiriwa kukamilika mwezi Februari mwakani.
Naibu Waziri Maji, Mh Amos Makalla akikagua ujenzi wa mradi maji
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ( aliyenyoosha mkono ) akiwa kwenye chanzo ziwa victoria eneo la Bukanga

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni