MABONDIA Vicent Mbilinyi na Kelvin Majiba wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika agost 22 katika viwanja vya mpira wa kikapu vilivyopo ndani ya shule ya Uhuru Wasichana Dar es salaam.
Mbali na mabondia hao kupima uzito, bondia mwingine bingwa wa WPBF na U.B.O Afrika Ibrahimu Class 'King Class mawe' nae amepima uzito kwa ajili ya mpambano wake na bondia kutoka mji kasoro bahari Ally Muhuro, na Fadhili Boika atapambana na Fransic Haule na Shomari Mirundi atakabiliana na Huseni Pendeza huku Roger Masawe akimkabili Raymond Mbwago.
Mipambano hiyo yote niya raundi sita sita. Akizungumza baada ya kupima uzito kwa mabondia hao, mratibu wa mpambano huo ambaye ni kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa siku hiyo mchezo utaanza mapema ili kuwapa watu wengi fursa ya kuangalia mipambano hiyo mikali zitakazokuwa na michezo takribani minne ya utanguliza
Mchezo huo una nia ya kukuza viwango vya mabondia nchini ili wapate uzoefu wa mchezo kupigana mara kwa mara.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni