Mkutano wa waandishi wa habari na
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ambao
aliutisha ili kutoa tamko lake umeahirishwa hii leo kutokana na kuwa
na kikao na wazee wa chama hicho kabla ya kuongea na waandishi.
Akizungumza katika ofisi za chama
hicho Jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bi. Magdalena
Sakaya amesema kuwa wamelazimika kuahirisha mkutano huo kutokana na
kikao kirefu baina ya Prof. Lipumba na wazee hao ambao wametaka
kujua anataka kutoa tamko gani kwa waandishi wa habari.
Kufuatia kauli hiyo waandishi wa
habari walilazimika kuondoka katika eneo la ofisi hizo huku baadhi ya
wanachama wa CUF, wakiendelea kuwepo nje ya ofisi zao wakidai
wanangojea kumuona Prof. Lipumba japo hata awasalimie baada ya
kumaliza kikao hicho.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni