Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya
boti mbili kugongana usiku wa jana kati ya visiwa vya Kiwa na Remba
katika ziwa Victoria eneo la Kenya.
Boti mojawapo inasemekana ilikuwa
imebeba wavuvi kutoka Rema kuelekea soko la Sori katika kaunti ya
Migori.
Ripoti za wavuvi katika fukwe ya
Nyandiwa katika kaunti ya Suba zinaonyesha kuwa watu tisa wamekufa
kutokana na janga hilo.
Kamishna wa polisi wa kaunti hiyo
John Omusanga amesema miili ya watoto wawili imepatikana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni