Licha ya Raheem Sterling kukosa
nafasi nzuri ya kuifungia goli kwa mara ya kwanza timu yake mpya ya
Manchester City dhidi ya West Brom lakini kwa mujibu wa mashabiki
wawili vijana wa timu hiyo kwao ni mchezaji bora wa mchezo huo.
Kufuatia ushindi mnono wa mabao 3-0
wa Manchester City dhidi ya West Brom, mchezaji huyo aliyesajiliwa
kwa kitita cha paundi 49 akitokea Liverpool aliruka mabango ya
matangazo na kuwapa jezi yake mashabiki vijana wawili.
Raheem Sterling alielekea kuwapa jezi mashabiki wa Manchester City
Ni furaha ilioje kupewa jezi na shujaa mpya wa Manchester City



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni