.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 6 Agosti 2015

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MZEE PETER KISUMO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo Upanga jijini Dar es salaam alipokwenda kwenye msiba wa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo, aliyefariki dunia Jumatatu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alikuwa anapatiwa matibabu8 ya figo. Marehemu Mzee Kisumo alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa Chama cha CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa wanasiasa wakongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo, aliyefariki dunia Jumatatu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alikuwa anapatiwa matibabu8 ya figo. Marehemu Mzee Kisumo alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa Chama cha CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni