Gareth Bale na James Rodriguez
wameifungia Real Madrid magoli mawili kila mmoja wakati timu hiyo
ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Real Betis katika ligi ya
La Liga.
Katika mchezo huo Gareth Bale
aliifungia Real Madrid bao la kwanza mnamo dakika ya pili tu ya
mchezo kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na James
Rodriguez.
Kipa wa Real Madrid Navas alionekana
kuwa shujaa mpya baada kuokoa mchomo katika kipindi cha kwanza na pia
katika kipindi cha pili alipomnyima bao Ruben Castro.
Gareth Bale akipiga mpira wa kichwa uliotinga wavuni na kuandika bao la kwanza
James Rodriguez akipiga shuti lililotinga wavuni



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni