Kwaya Maalum ya Jangwani kutoka Shinyanga ikitumbuiza wakati wa Sherehe za Makambi ya Mtaa wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese .
Kwaya ya Angaza ikimwimbia Mungu siku ya kuhitimisha sherehe za makambi Manzese. PICHA ZOTE NA SARAH REUBEN
Sherehe za Makambi kwa mwaka 2015 katika Mtaa wa Manzese zimemalizika kwa kishindo cha kubatiza waumini ishirini na saba (27) ambao wameamua kumpokea Yesu kwa kujiunga na kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.
Akizungumza na waumini wa kanisa hilo wakati wa kuhitimisha sherehe hizo mwishoni mwa wiki, Mchungaji Idelphonce Tirumanywa amesisitiza kuwa kanisa kuendelea kuwalea vyema waumini wapya waliojiunga na kanisa hilo.
Mch. Tirumanywa pia ameendelea kuwaasa waumini wote wa kanisa la waadventista wasabato kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuonesha matendo mema yatakayo warudisha watoto wa Mungu waliopotea nyumbani.
“Ni wakati wakurudi nyumbani, dunia ipo kwenye hatari kubwa, tena kubwa sana. Tunapoishukuru serikali yetu kwa uhuru wa kuabudu, waadventista wasabato wote amkeni muumtangaze Mungu ili watoto wa Mungu waache dhambi na kurudi nyumbani”, alisistiza Mch. Tirumanywa.
Sherehe za makambi ya mtaa wa Manzese yalihudumiwa na kwaya maalum kutoka Sauti ya Jangwani Shinyanga wakishirikiana na kwaya tatu (3) zinazounda mtaa huo yaani Angaza, Mbiu na Sauti ya Nyikani zote kutoka Dar es Salaam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni