Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) linatoa pongezi za dhati kwa Rais wa Shirikisho ndugu ROBERT MUTA RWAKATALE kuchaguliwa mgombea udiwani kupitia CCM. Katika Kikao cha kamati ya utendaji cha (BFT) kilichofanyika katika Ofisi za BFT kiliomba kumpongeza Rwakatale kwa nafasi hiyo aliyoipata kupitia chama cha CCM kwa kuchaguliwa kugombea Udiwani KAWE.
BFT. Ina Imani kubwa na uongozi wa MUTA RWAKATALE kwa kuwa amekuwa Imara kuhakikisha kuwa BFT inasonga mbele ingawa kuna changamoto mbalimbali za kuongoza vyama vya michezo.
(BFT ) inaamini kuwa endapo atachaguliwa kuwa Diwani KAWE atashirikikana na Madiwa wa Kata nyingine pamoja na Mbunge wa Kawe kuleta maendeleo ya haraka katika Jimbo la KAWE.
MUTA RWAKATALE amechaguliwa kwa kuwashinda vigogo waliogombea nafasi hiyo kama alivyokuwa MEYA wa Manispaaa Kinondoni kwa miaka (10) na mjumbe wa NEC SALUM LONDA, OTHMAN KIPETA- Diwani ambaye amemaliza muda wake kwa sasa na Lokelo Willilo Makamu wa Rais (BFT).
MAKORE MASHAGA
KATIBU MKUU ( BFT)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni