Ugonjwa wa kipindupindu umezidi
kushika kasi Jijini Dar es Salaam tangu kutokea mlipuko wake mwishoni
mwa wiki iliyopita ambapo sasa idadi ya wagonjwa imeongezeka kutoka
wagonjwa 36 jana na kufikia wagonjwa 40 leo.
Kufuatia hali hiyo Mganga Mkuu wa
Manispaa ya Kinondoni Bw. Aziz Msuya amesema manispaa hiyo imeanza
zoezi la kuwaondoa wauza vyakula vya kupikwa wanaouza vyakula vyao
karibu na maeneo yanayotiririka maji machafu.
Aidha, Bw. Aziz amewataka wananchi
kumuwahisha hospitali mara moja mgonjwa yeyote ambaye atabainika
kutapika na kuharisha mfululizo ili aweze kupatiwa matibabu ya
haraka.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni