Umoja wa Mataifa umesema upo tayari
kuchukua hatua, iwapo rais wa Sudani Kusini Salva Kiir hajatia saini
makubaliano ya amani na waasi.
Kiir anatarajiwa kutia saini
makubaliano ya kumaliza miezi kadhaa ya vita ya kikatili hii leo,
kiongozi wa waasi Riek Machar alitia saini makubaliano hayo wiki
iliyopita.
Mapigano baina ya vikosi vitiifu vya
viongozi hao wawili vimepelekea watu milioni 2.2 kukosa makazi.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni