Utoaji mimba holela umeongezeka
nchini Kenya, ambapo watoaji mimba wasionasifa husababisha vifo vya
wanawake 2,600 kila mwaka idadi ambayo ni kubwa kuliko hata ya vifo
vitokanavyo na saratani ya shingo ya uzazi nchini humo.
Wizara ya Afya ya Kenya imesema
karibu matukio laki tano yautoaji mimba hufanywa nchini Kenya kila
mwaka, ambapo kati ya hayo 375,000 hufanyika vichochoroni.
Timu ya Wataalam wa Afya ikiongozwa
Joyce Mumah wa Shirika la Utafiti la Idadi ya Watu Afrika (APHRC),
imesema watoaji mimba wasionasifa sio tu huuwa wanawake 2,600 pia
huwaachia majeraha ya kudumu.
Mwaka jana wanawake 2,451 nchini
Kenya walikufa kwa saratani ya shingo ya uzazi kwa mujibu wa Shirika
la Afya Duniani (WHO).

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni