Wimbi
la mashambulizi limeikumba nchi ya Uturuki hii leo, ambapo maafisa
polisi wanne wameuwawa kusini mashariki mwa nchi hiyo huku mlipuko wa
bomu ukitokea katika Jiji la Istanbul.
Kwa
nyakati tofauti, washambuliaji wawili wenye silaha walifyatua risasi
nje ya ofisi ndogo ya Ubalozi wa Marekani huko Istanbul, hata hivyo
hakuna hata mtu mmoja aliyejeruhiwa.
Maafisa
polisi wanne wameuwawa kwa mlipuko katika barabara ya mkoa wa Sirnak,
muda mfupi tu baada ya wapiganaji kufyatulia risasi helkopta ya jeshi
na kumuua mwanajeshi mmoja.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni