Mshambuliaji kinda Anthony Martial
ameandika historia ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kununuliwa kwa
bei mpaya kuliko wote duniani baada ya kutwaliwa na Manchester United
akitokea Monaco.
Ada ya mchezaji huyo Mfaransa mwenye
umri wa miaka 19 anayefananishwa na Thierry Henry ni paundi milioni
36, na huenda ikaongezeka hadi kufikia paundi milioni 58 kama mambo
yake yatakuwa safi.
Kitita hicho kinazidi rekodi ya
paundi milioni 32 ilizotoa timu ya Paris Saint-Germain kwa Sao Paulo
ya Brazil kumnunua mshambuliaji kinda Lucas Moura miaka mitatu
iliyopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni