Wahamiaji wawili kutoka nchi za
Afrika Magharibi, wameingia eneo la Hispania la Ceuta wakitokea
Morocco wakiwa wamejichimbia kwenye eneo la injini ya gari na nyuma
ya kiti cha nyuma cha gari aina ya Mercedes-300.
Polisi nchini Hispania iliwabaini
watu hao siku ya jumapili wakati maafisa forodha wakifanya ukaguzi
katika mpaka wa El Tarajal, karibu na mpaka wa Moroccan.
Wahamiaji hao wawili wote wanaume
wanatokea Guinea walipatiwa huduma ya kwanza kutokana na kukosa hewa
ya oxygen, maafisa polisi wa eneo la Guardia nchini Hispania
wamesema.
Mhamiaji akiwa amejificha eneo la injini ya gari
Huyu mwingine alikutwa nyuma ya kiti cha gari
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni