Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa
Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wananchi na wana CCM wa Kijiji
cha Mitambuuni alipofika kuwasailia akiwa katika ziara ya Kisiwa cha
Pemba.
Balozi Seif akisalimiana na
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Kijiji cha Mitambuuni Wete Mkoa
wa Kaskazini Pemba, kulia yake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini
Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa na kushoto yake ni Mjumbe wa Kamati ya
Siasa ya CCM ya Mkoa huo Omar Khamis Othman.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha
Mapinduzi wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati
akizungumza na wana CCM na Vijana wa Maskani ya Vumilia ya Mitambuuni
Wete Pemba.
Baadhi ya Wana CCM na Wananachi wa
Kijiji cha Miktambuuni Wete Pemba wakihamasiska kumlaki Mjumbe wa
Kamat Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif akiwapongeza Vijana wa
Maskani ya CCM YA Vumilia ya Kijiji cha Mitambuuni baada ya kuamua
kuuhama upinzani na kujiunga na Chama cha Mapinduzi.
Press Release:-
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri
Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi alisema
kwamba ni aibu kubwa kuona Wananchi wa Kijiji cha Mitambuuni kiliopo
Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wanakosa huduma za Skuli ya
Maandalizi kwa watoto wao wakati Wawakilishi na Wabunge wao wapo.
Alisema inasikitisha na kutia
uchungu kutokana na kadhia inayowapata watoto wa Kijiji hicho ya
kufuata masomo umbali wa kilomita Sita matatizo ambayo yanaweza
kupatiwa ufumbuzi ndani ya uwezo wa Viongozi wao wa Jimbo.
Balozi Seif Ali Iddi alielezea
masikitiko yake wakati wa hafla fupi ya kuizindua Maskani ya CCM ya
Vumilia ya Kijiji cha Mitambuuni Mkoa wa Kaskazini Pemba
iliyoanzishwa na Vijana walioamua kuacha upinzani na kujiunga na
Chama cha Mapinduzi .
Alisema Chama cha Mapinduzi katika
kipindi kijacho mara baada ya uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba
kinakusudia kufanya mabadiliko zaidi ya Maendeleo katika Majimbo la
Kisiwa cha Pemba kwa lengo la kupunguza kero zinazowakabili Wananchi
wa Majimbo hayo.
Balozi Seif aliwakumbusha na
kuwaomba Wananchi wa Majimbo ya Kisiwa cha Pemba kuhakikisha kwamba
wanawachagua Viongozi watakaokuwa tayari kufanya kazi nao.
Alisema wapo viongozi wengi wa
Majimbo hayo wenye tabia ya kuyahama majimbo yao mara tuu bada ya
kuchaguliwa na kuazisha Familia nyengine katika maeneo ya Unguja, Dar
es salaam na Dodoma na kusahau kwamba wamebeba dhima ya kuwatumikia
wananchi waliowapa kura zao.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwapongeza Vijana hao wa Kijiji cha
Mitambuuni kwa uamuzi wao wa kufuata sera sahihi zinazotekelezeka za
Chama tawala cha Mapinduzi.
Balozi Seif liwataka Vijana hao kwa
kushirikiana na Wazazi na Viongozi wa eneo hilo kuanza maandalizi ya
ujenzi wa maskani yao ya kudumu pamoja na Skuli ya Maandalizi kwa
hatua ya msingi
Aliwahakikishia wananchi na Vijana
hao wa Mitambuuni kwamba atachukuwa juhudi za makusudi katika kuunga
mkono uendelezaji wa ujenzi wa majengo yote Mawili ili kusaidia
kuwaondoshea changamoto zinazowakabili watoto na Vijana hao.
Mapema Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa alisema
Mtambwe na Vitongoji vyake imebadilika kutokana na Sera sahihi za
Chama cha Mapinduzi zilizokuwa zikitekelezwa na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Mzee Mberwa alisema harakati za
kiuchumi zimeongezeka na kupanuka mara dufu na kutoa fursa pana
zaidi kwa Wananchi maeneo hayo kuendeleza vyema maisha yao ya kila
baada ya kukamilika kwa miundo mbinu bora ya mawasiliano ya bara
bara.
Akisoma Risala ya Maskani hiyo ya
CCM ya Vumilia Mitambuuni Katibu wa Maskani hiyo Ndugu Juma Said
Saleh alisema uamuzi wa vijana hao kuuhama upinzani na kuhamia CCM
unatokana na tabia ya viongozi wanaowachaguwa kutokujali
kuwatumikia.
Nd. Said alisema dharau ZA Viongozi
hao zimesababisha kuibuka kwa changamoto kadhaa zisizopaswa
kutatuliwa na Serikali Kuu ambazo zimo ndani ya uwezo kamili wa
Viongozi wao wa Majimbo.
Katibu huyo wa Maskani ya Vumilia
alieleza kwamba Vijana hao katika kupambana na tabia ya Viongozi hao
wameahidi kufanya kampeni ya nyumba hadi nyumba katika kuhakikisha
Wagombea Uchaguzi kupitia Chama cha Mapinduzi wanaibuka washindi ili
waweze kuwatumikia kwa upendo na ushirikiano.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
9/9/2015.1





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni