Timu ya Chelsea wakicheza nyumbani
wamepata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv katika mchezo
wao wa kwanza wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo mabao yakifungwa
na Williani,Oscar, Diego Costa na kiungo Cerc Fàbregas akikamilisha
karamu ya mabao.
Fabregas akipachika bao la nne la Chelsea
Nayo Arsenal ilijikuta ikianza
vibaya michuano hiyo kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya
Dinamo Zagreb, huku mshambuliaji wao Olivier Giroud akitolewa nje kwa
kadi nyekundu.
Refa akiitafuta mfukoni kadi nyekundu ya kumpa Oliver Giroud
Mpira si lelemama wanaume wakiwa kazini
Nchini Italia timu ya Roma wakiwa
wenyeji wa Barcelona wamekwenda sare ya kufunga bao 1-1, mabao
yakifungwa na Suarez kwa Barcelona na Florenzi kwa upande wa Roma.
Matokeo ya michezo mingine
iliyopigwa jana Bayer Leverkusen 4 -1 Bate Bor, Olympiakos 0-3 Bayern
Mun, Dynamo Kiev2 - 2FC Porto, KAA Gent 1 -1 Lyon na Valencia 2- 3
Zenit St P.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni