Magufuli amewataka Wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Aidha hadi jana, tarehe 16 September 2015,
Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya
kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa
ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari,
jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na
asilimia zaidi ya 30 ya wapiga
kura.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni